SIMULIZI MPYA "DE LIFE I DESERVE"

Dampa

JF-Expert Member
May 29, 2017
810
1,263
Hello guyz Mamboooz....
Nakuja na stori mpya kabisa ya kusimumua na kufundisha iliyojaa visa vya kifamilia pamoja na kimtaa mtaa...
Imeandikwa kwa mpangilio mzuri lugha nzuri itakayokufanya usichoke kuisoma. Whoooo....! Now forget about sijui penny sijui nani check bonge moja la stori kutoka kwngu DAMPA AU DROPA
Nitadrop the stori everyday so itz gonna be lit ...
Wasitue wapenzi wote nowu
 
Shigongo anahamia jf
Taratibu

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
DE LIFE I DESERVE PART 1

Basi bhana baada ya kuachana na mama na maneno yake ya kila siku kuhusu kutafuta kazi kuliko kushinda kwenye vilinge na masela na wana,Nikazama gheto kwangu huku nimechoka na kinjaa uzembe kikizidi kulisokota tumbo langu.Lengo halikuwa kulala wala nn ....Yalaaah ! Kumbe dg P kasepa nayo.Nilijisemea kimoyo moyo baada ya kukuta buku langu halipo juu ya meza .Itakuwa dg P tu kaondoka nalo.Mama yangu hapo ndo njaa ikawa kama imetiwa ndimu na pilipili mpaka nikajikuta najuta kwanini asubuhi nilimchenga mshua aliponipa deal ya kuosha gari yake.

Lakini sio kesi sababu hata mimi huwa namchapa sana dg vibuku buku vyake wakati sina nauli ya kwendea town kwenye amshaamsha zangu.Dogo langu nampenda sana tunaishi km tupo mbele kwa love tunayooneshana. Ni mcheshi,mpole ,hardworking na hapendi mambo ya kijinga jinga yani kum-face inabidi ujipange lasivyo atakuaibisha cz he is a good thinker. Ni mdogo Kiumri (14) lakini ana busara kama mtu mzima japo yupo darasa la 5.

Wakati nikiwaza na kupotezwa katika wimbi la mawazo lilochanganyika na kinjaa flan hv amaizing,Ilikuwa yapata kama saa saba kasoro hv nilishitushwa na mlio wa simu yangu kuashiria kuna ujumbe umeingia.Aagh nikaupuuzia nikijua ni voda tu hao wananidai wananikumbusha deni lao cz inakaribia kukata mwezi sasa sijaweka vocha toka nikope.Zaidi anayeniokoa ni demu wangu wa chuo ambaye huniungia kifurushi pale asiniona online.

Oooooh men wtf ! ,sema kibishi tu mzee bhabha nakomaa.Heee ! Eeeh ndo hivyo usawa wenyewe ndo kama huu basi nikaichukua simu kizembe zembe toka kwenye charge kisha nikajibwaga kitandani huku nashauku ya kujua ujumbe unasema vp.Lakini kabla sijafungua nikasikia maza ananiita kwa sauti ya juu na ya ukali,in short mim na bi mkubwa huwa tunapelekana kibabe sana kiupande wake hanikubali sana kama anavyonikubali mshua so most of the time tunalumbana hapa na pale but all in all tunapendana sana.

Nadhani sijui ni tabia yangu kutopenda kuingiliwa kwenye maamuzi yangu especially Mwanamke ndo kitu ambacho tunalumbana sana na bi mkubwa si kwamba namdharau lakini ni kitu ambacho kiko ndani yangu hata yeye analijua hilo.Mara kadhaa huwa anasema nina tabia kama za baba yake ambaye ni babu yangu,basi mimi huishia kucheka tu ndo hapo anafura tu kisha namtania kwann Mama yake aliweza kuishi na babu yeye atashindwa vp kama ni hivyo mama hubaki anatabasamu halfu nammaliza kwa kumwambia aniite baba.In short Family yetu tunapendana sana najivunia kwa hilo aiiise.

Basi bwana Ghafla nikaibuliwa kwenye lindi hilo na makelele ya mama huku anagonga mlango kwa nguvu sana mpaka nikapatwa na hofu.Wakati mwanzo anaanza kugonga nilichukulia kawaida tu sababu nilisha mzoea mama gonga yake ni ya fujo anaponihitaji nikiwa gheto lakini leo alinitia hofu sana cz siyo kawaida..

Kwa kasi ya ajabu nikasimama nakushika funguo cz ninapoingia gheto mm lazima nitie funguo kabisa.Ghafla nikaminya kitasa mlango ukafunguka,nikapigwa butwaa nilichokiona mbele ya macho yangu sikuamini..........!!!



Je nn nilikiona fuatana nami next time usisahau kushare kukoment na kutukana pia unaruhusiwa ila siyo ya nguoni.....Natania

Tchaooooo.!!!?

By Dampa
 
DE LIFE I DESERVE PART 2

Nikajikuta naropoka kwa sauti what de hell is this....! Ni mdogo wangu wakike Jane ambaye sauti hata na umbo wamefanana sana na mama,Namkuta anachezesha macho na pua just like this video down below.na kwa staili ya kunitisha kama alivyozoea masihara yake.Kidogo nilichukia cz nilipigwa na butwaa sana nilihisi huenda mama kapatwa na majanga kumbe ni hiki kidudu mtu.Nilitamani nimtie kibao ila nafsi ikanisuta cz hata mimi ndo michezo yangu hiyo. Nilijikuta natabasamu ili kuobyesha sijachukia au hajanistua sana japo moyoni nilijaa sumu vibaya.
"Haaa haa haa hii ahiii huyo nimemweza leo mama Dick analia heee hiii njoo umuone"
Jane alisema huku anakimbia kuelekea jikoni kumbe msosi ulikuwa tayari na mama alijua njaa ilivyonikamata so waliamua kunichezea cz wanajua navyokuwa nikiwa na njaa.
Acha hiyo kuna vituko vingi sana hutokea hapa kati yetu ambavyo hutufanya tuwe close sana kwenye familia yetu.
Baada ya vicheko na mishushuo ya hapa na pale kati yet,nilienda jikoni nakuchukua msosi wa kutosha kama kawaida yangu.
Baada ya kula ndipo nikakumbuka kuna ujumbe ulingia kwenye simu yangu fasta nikakimbilia chumbani kwangu,nikachukua simu nakufungua ujumbe. Nikausoma japo ilikuwa no ngeni ila ujumbe ulisomeka hivi.
"Usikose kufika TopCity pub kimara kuanzia saa nne usiku"
Duh nikapigwa na butwaa nikawaza huyu atakuwa nani na anataka nn ikabidi nimuulize lakini hakujibu nikatuma tena sms kama 2 ila zote kimya.Nikajua labda jamaa flani tu ka wrong namba.Nikaipotezea simu nikaweka chaji nakufanya shughuli nyingine.
Baada ya muda kidogo wazo likanituma niipige Nikapiga lakini haikuita wala nn mara ghafla ndo nikajuwa hata namba hazikuwa za nchi hii.Nikaangalia code yake ni number ya marekani ....! Heeee cz ilikuwa +1..............nikajaribu kuipotezea lakini bado akili haikutaka.Mwisho nikapitiwa na usingizi nikalala.
Saa kumi na mbili jioni katikati ya usingizi mwepesi wa mchana nikajiona kama niko vitani napigana na wanajeshi kwenye ndoto narusha mabomu ya vifaru si unajua venye vita inaenda.
Mara nikajiona nipo kwenye helikopta narusha mabomu kwa chini huku napiga mikelele kibao,ghafla kwa mbele nikaona kama bomu linanifuata nikajaribu kukwepa lakini ikawa late nikaripuka na kutoa ukelele mkubwa sana BOOOOOOOOOOOOMMMMM...... !.Nikastuka toka usingizini ghafla hee nikamkuta dg p anapiga mikelele kama niliyopiga kwenye ndoto ,Yalaaah kumbe alikuwa anacheza computa game ya kivita halafu sauti iko juu sana.Kumbe ndoto ilingiliana na game so nikawa km mm ndo nipo kwenye vita.
Hii kitu inaitwa brain function bhana, brain inabadili mazingira mtu aliyopo na kuyafanya km ndoto pale mtu anapolala usingizi mwepesi,Kwa mfano ukilala karibu na radio inapiga mziki ukilala unaweza hisi wew ndo unaimba hiyo nyimbo kumbe ndoto tu.Noma sana haya mambo ya kisayansi broo.
Dg P alihisi kaniamsha akapologize nikamwambia its fine,Akaniambia bro halafu simu yako imeita sana ila no ngeni.Nikajua ndo ile ile nikawahi kuchukia simu kucheck kuna missed call tatu na jumbe nne mbili za hii no +1........
Ujumbe mmoja ulisema ""Usikose kufika TopCity pub kimara kuanzia saa nne usiku"
Na wapili ulisema ukifika piga hii no namba kwa maelezo zaidi but inapatikana kwenye eneo hilo tu.........
Mh nikashangaa na kuchanganyikiwa kabisa sana .......


Je ni nani hawa na nn kitatokea fuatana na story ndo kwanza inaanza cz hata msimuliaji bado hatujamjua vizuri so keep it up more to come......
See ya next time
Tchaooooo
By Dampa
 

Attachments

  • 51a65f6e.mp4
    769.9 KB · Views: 29
Back
Top Bottom